Isaiah 54:6-8


6 a Bwana atakuita urudi
kana kwamba ulikuwa mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni;
kama mke aliyeolewa bado angali kijana
na kukataliwa,” asema Mungu wako.

7 b“Kwa kitambo kidogo nilikuacha,
lakini kwa huruma nyingi nitakurudisha.

8 cKatika ukali wa hasira
nilikuficha uso wangu kwa kitambo,
lakini kwa fadhili za milele
nitakuwa na huruma juu yako,”
asema Bwana Mkombozi wako.

Copyright information for SwhKC